Ilikuwa ni jumapili njema yenye miujiza na nguvu ya Mungu isiyo yakawaida..
Kadri imani inavyoongezaka ndani ya mtu ndivyo majaribu yanavyozidi kuongezeka katika maisha ya mtu..Ikimwanini Yesu kristo hakuna jaribu litakalokushinda.
1 kor 10:13
Jaribu halikuwapata ninyi,isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wakutokea,ili mweze kustahimili
Haijalishi unapitia katika jaribu gani,yawezekana ukawaunapita katika kipindi kigumu sana cha uchumi au kipindi kigumu cha ndoa yako, au kipindi kigumu cha afya yako, magonjwa yamekuandama hata madaktari wamekukatisha tamaa kuwa hutapona tena ila lipo jambo moja tu unalotakiwa kulifahamu,Mwamini Yesu kristo mwana wa Mungu aliye hai, aliyekufa msalabani kwaajili yako alibeba mizigo yako ili upate kuwa huru, Na kwakupigwa kwake ulipata kupona,Hakuna jambo gumu Mungu asiloweza kufanya,wala mzigo mzito Mungu asioweza kuubeba,Mkimbilie yeye ndoye mwamba wa uzima wako..
No comments:
Post a Comment