PASTOR MYAMBA FILMS

Wednesday, November 17, 2010

NINI HATMA YA SANAA YA FILAMU TANZANIA (sehemu ya 1)

Nimekuwa nikifikiri kila siku pasipo kupata jibu la nini hatma ya sanaa ya filamu ya Tanzania,Wasanii ni kati ya watu wanaoishi maisha ya kiwango cha chini kabisa kuliko mtu yeyote anaefanya kazi sehemu nyingine tu mtaani,Soko la filamu limeshikiriwa na wahindi wasiojua sanaa yoyote ile,imefikia kipindi wasanii wanapokea maelekezo ya nini chakufanya katika filamu kutoka kwa muhindi asiyejua chochote katika sanaa,na unakuta huyu muhindi anatoa maelekezo yakuua uhalisi wa sanaa lakini inakubidi ufuate maelekezo hayo kwani yeye ndie mnunuzi..Mfano Muhindi anataka filamu iwe na wanaume weupe,kitu ambacho hakina msingi katika sanaa na hii hupelekea hata wasanii wengi kujichubua ili kufit maagizo ya huyu muhindi ambae hata kiswahili hajui vizuri, Je nini hatma ya sanaa yetu?.

No comments:

Post a Comment